Ahadi za wengine ni maigizo tu

MCHINGA : MGOMBEA wa urais kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM), Rais Samia Suluhu HassanĀ  amewataka kukiamini sera za chama chake na kusisiza za wengine ni za kuigiza tu.

Akizungumza na maelfu.ya wananchi waliofurika katika Jimbo la Mchinga, Samia alisema: “lakini nataka niwaambie hakuna chama kitakachoweza kwa sasa hivi kulinda na kuinua utu wa Mtanzania kama Chama cha Mapinduzi, na ndiyo maana tumekuja na hii kauli mbiu ya kazi na utu. Maana yake tupeni ridhaa yenu chama cha mapinduzi tuendeshe nchi hii tena kwa miaka mitano ijayo.”

“Huko mbele tutakuja tena kutufanyia tathmini, tufanye kazi ili tuinue utu wa mtanzania na katika kuinua utu wa mtanzania ni kumpatia majisafi na salama, elimu, huduma za afya, umeme, kilimo, huo ndiyo kulinda na kuukuza utu wa mtu. Ukisoma ilani yetu yote tunakwenda kufanyakazi ya kukuza na kuulinda utu wa mtanzania tu wa mwananchi.” SOMA: Wagombea udiwani Ngorongoro waomba bajeti kusukuma miradi

“Wengine wanapitia ilani yetu wanadokoa dokoa, wanasema tutatoa elimu bure kwani CCM haijatoa?, tunatoa msingi mpaka kidato cha sita na pia kuna fungu la mkopo ukienda chuo kikuu tunakwambia kopa hapa kijana kasome ukipata kazi, ukijiajiri utarudisha polepole.”

Samia aliongeza: “mwingine anakwambieni nitaleta maji, alikuwa wapi asilete siku zote. CCM tumeshaleta maji. Kwa hiyo ahadi zao ni za kuigiza tu. Niwaombe sana wananchi Oktoba 29 nendeni mkachague Chama cha Mapinduzi.”

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button