Airtel, Tecno wapeleka wanne Afcon

KAMPUNI ya mtandao wa simu ya Airtel Tanzania kwa kushirikiana na TECNO, imepeleka washindi wanne nchini Ivory Coast kushuhudia fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON 2023) kati ya wenyeji Ivory Coast dhidi ya Nigeria kesho.

Washindi hao ni Marcel Leonard, Jafari Salukele, Alfred Mlita, na John Kimario waliowasili jana ambapo watashuhudia mchezo wa fainali kati ya Nigeria na Ivory Coast kwenye Uwanja wa Alassane Outtara.

Mkurugezi wa Airtel Money, Andrew Mugamba amesema nafasi hiyo imetokana na washindi hao kushiriki katika promosheni ya siku 90, ‘Upige Mwingi Mpaka AFCON’ ambayo imetengenezwa kuwazawadia wateja wao zawadi mbalimbali zikiwemo simu janja ya Tecno Spark 20, Jokofu, TV, bodaboda pamoja na vifurushi vya data, dakika na SMS.

Advertisement

“Promosheni ya ‘Upige Mwingi mpaka AFCON’ inaonesha dhahiri jinsi Airtel Tanzania inavyojitolea kufikisha huduma nzuri kwa wateja wake Pamoja na kuwapa kumbukumbu zisizosahaulika,”amesema.

Alisema ushirikiano wa Airtel Tanzania’ na TECNO umekuwa muhimu katika safari hii, ukilenga kuongeza uwezo wa kupenya kwa simu mahiri za bei nafuu na zenye ubora kama vile Tecno Spark 20 zipatikane kwa wateja.
“Ushirikiano huu unasisitiza zaidi maono ya pamoja ya kuvunja mipaka katika michezo na teknolojia, na kuwahimiza wateja wa Airtel kuota ndoto kubwa na kufikia uwezo wao kamili,”ameongeza.

“Tunawahimiza wateja zaidi kushiriki katika ofa ya Upige Mwingi kwani kuna zawadi zaidi za kushinda.” Alisema Mugamba.

Kwa upande wake Jafari Salukele, mjasiriamali na mmoja wa washindi alisema, “Nimefurahi sana na ninashukuru kwa fursa hii ya mara moja maishani kushuhudia fainali za AFCON 2023 moja kwa moja nchini Ivory Coast,”