Al Ahly waingia 18 za Simba

DAR ES SALAAM: WAPINZANI wa Simba SC katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL), Al Ahly SC imewasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu nchini Misri na CAFCL wamepost video inayoonesha wakiwasili huku ikichagizwa na maneno “Habari, Tanzania 👋🇹🇿”.

Mnyama Simba atakabiliana na mashetani hao wekundu mnamo Machi 29 mwaka huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Mchezo wa marudiano unatarajiwa kupigwa Aprili 05 nchini Misri saa 5:00 usiku.

Habari Zifananazo

Back to top button