Ali Hapi azungumzia serikali inavyotengeneza ajira

DAR ES SALAAM: Takwimu zinaonesha kuwa katika miaka mitano iliyopita, Serikali imetengeneza ajira rasmi na zisizo rasmi milioni 8 nchi nzima.

Hata hivyo, ili kujenga uchumi jumuishi na fungamanishi, ni muhimu kuelewa kuwa asilimia 75 hadi 80 ya watu nchini ni wakulima wanaotegemea kilimo kama nyenzo kuu ya kiuchumi.

Katika juhudi za kuendeleza kundi hili kubwa la wakulima, Serikali imeongeza matumizi ya mbolea katika kilimo. Miaka minne hadi mitano iliyopita, matumizi ya mbolea yalikuwa tani 580,000 kwa mwaka, lakini sasa yameongezeka hadi tani milioni 1.112 kwa mwaka. Hii inaashiria jitihada kubwa katika kuinua uzalishaji wa kilimo.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ali Hapi, amebainisha kuwa matumizi ya mbolea ni kiashiria kikubwa kinachoonyesha hali ya uchumi wa kilimo.

“Nchi yetu bado ina kiwango cha chini cha matumizi ya mbolea ikilinganishwa na uwezo wake, hivyo tunahitaji kufanya vizuri zaidi ili kuhakikisha wakulima wanapata mavuno bora na uchumi wetu unakua kwa nguvu,” amesema.

Aidha, juhudi hizi za Serikali zinaendelea kusaidia kuimarisha sekta ya kilimo, kuongeza ajira, na kusaidia kuinua hali ya maisha ya wakulima wengi nchini.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button