Amina Jigge aipeperusha Bendera ya Tanzania Miss Earth 2025

MREMBO wa Tanzania, Miss Amina Jigge, amepewa heshima ya kuiwakilisha nchi kwenye mashindano makubwa ya urembo duniani, Miss Earth 2025, yanayofanyika nchini Ufilipino. Amina, ambaye kwa sasa yuko kambini rasmi na warembo wengine kutoka mataifa mbalimbali, ameonesha ari na dhamira ya kuipa Tanzania heshima katika jukwaa hilo la kimataifa.
Akizungumza na Habari leo Amina kabla ya kuanza kwa mashindano hayo, Miss Amina Jigge amewaomba Watanzania kumpa sapoti na dua, akisisitiza kuwa atatumia nafasi hiyo kutangaza utalii na utamaduni wa Tanzania. Ninajivunia kupeperusha bendera ya Taifa langu. Naomba Watanzania wote waniunge mkono.




