Arusha wamshukuru Samia vipimo magonjwa ya moyo

ARUSHA; Wananchi wa Mkoa wa Arusha na mikoa ya jirani wamemshukuru Rais wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan kwa uwezeshaji wake wa programu ya vipimo na matibabu bure kwa magonjwa ya moyo inayofanyika kwa ushirikiano Kati ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Hospitali ya Arusha Lutheran Centre (Seliani).

Leo Jumanne Januari 6, 2025 wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Makalla ya kukagua tukio la matibabu, amesema ujenzi wa Kituo cha JKCI katika Hospitali hiyo kutasaidia pia wananchi, watalii pamoja na washiriki wa michuano ya Mpira wa miguu kwa mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027 kituo cha Arusha.

Kwa mujibu wa Makalla jumla ya wananchi takribani 1,200 wamenufaika na huduma hiyo ya matibabu bure, akiahidi kwamba serikali itawawezesha wananchi wasiokuwa na uwezo na waliopewa rufaa ya kwenda kutibiwa zaidi kwenye Taasisi ya Moyo JKCI  jijini Dar es Salaam pamoja na kuhamasisha wananchi umuhimu wa Bima ya Afya kwa wote.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button