Askofu Mwela ataka uadilifu watumishi wa umma

MBEYA;  ASKOFU Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Nyanda za Juu Kusini, John Mwela amewataka watumishi wa umma kuzingatia uadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao.

Ametoa kauli hiyo kwenye mahubiri ya Misa takatifu iliyofanyika Jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Stephano la Isanga, Mbeya.

Amesema ni muhimu watumishi wa umma wakiwemo viongozi kuzingatia miiko na maadili ya kazi zao, huku wakijawa na upendo kwa watu wanaowaongoza.

Amesema kumtanguliza Mungu kwenye utendaji kazi wao ni njia sahihi ya kuwafanya kuwa wanyoofu na wenye kusikiliza mahitaji ya wanyonge na kuyatafutia ufumbuzi.

“Kuongoza watu ni pamoja na kuwasikiliza. Kiongozi uongoze kwa uadilifu watu wakukimbilie na usie mwiba watu wakukimbie,”amesema Askofu Mwela.

Askofu huyo pia aliwasihi waumini wa kanisa hilo kuzingatia maagizo ya Mungu hatua aliyosema itawawezesha kupata mafaniko maishani mwao.

Amesema waumini wanapotoa sadaka mbele za Mungu ni muhimu wakazisemea, ili ziwe zenye maana iliyo na uzito na zenye kufikisha ujumbe kwake.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button