Babati vijijini kumenoga ufunguzi wa kampeni

KAGERA: Kampeni za Uchaguzi Mkuu zilizoanza Agosti 28 mwaka huu zitamalizika Oktoba 28 na upigaji kura utafanyika Oktoba 29 ambapo watanzania watamchagua Rais, wabunge na madiwani watakaohudumu kwa kipindi cha miaka mitano hadi 2030.

Katika uzinduzi wa kampeni za Jimbo la Babati vijijini ambazo zimefunguliwa katika Kata ya Mamire ambapo aliyekuwa diwani wa kata hiyo akiwa CCM na kufanya maamuzi ya kuhama chama kuingia ACT baada ya jina lake kukatwa ndipo Babati Vijijini kuamua kufanya uzinduzi kwenye kata hiyo ili  waweze kuwahasa wananchi wasishawishiwe kuchagua chama kingine tofauti na CCM ili maendeleo yazidi kumiminika kwenye kata yao .

Kwa upande wake mgombea wa ubunge wa jimbo la Babati vijijini, Daniel Baran Sillo ameomba kuchaguliwa ili aendelee kusaidia na serikali kuleta maendeleo kwa wananchi.

Katika uzinduzi huo alikuwepo aliyekuwa mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na sasa kuhamia Chama cha mapinduzi (CCM) Cecilia Daniel Paresso amewataka wananchi wa jimbo la Babati Vijijini kumchagua mgombea urais wa chama hicho Dk Samia Suluhu Hassan.

“Samia Suluhu Hassan ametuambia akienda ofisini ataenda kuhakikisha wagonjwa wa saratani wagonjwa wa sukari na figo wanagharamiwa na serikali kama haitoshi amesema kwenye sekta ya afya na sekta ya elimu atatoa ajira takribani kwa vijana 12,000, “amesema Cecilia.

Naye Mgombe ubunge Jimbo la Hanang, Asia Halamga amesema jambo lao ni moja tuu ni maendeleo na wamekubaliana kutoa kura za ndio za kutosha na watakuwa wa kwanza kitaifa kumchagua Dk Samia Suluhu Hassan.

Mbunge mteule wa UWT Mkoa wa Manyara, Regina Ndege amewasihi wananchi kutofanya makosa siku ya uchaguzi “wananchi wa Babati vijijini tumeona wageni wanavyomsemea Dk Samia Suluhu Hassan mmesikia wakimsemea Daniel Sillo lakini siyo hilo tuu na mimi niungane na wenza wote kusema kuwa chaguo pekee siku ya Oktober 29 ni CCM.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button