Banda la Mama waita vijana kupiga kura

MRATIBU wa kampeni ya Banda la Mama, Mhandisi Aivan Maganza, ametoa wito kwa Watanzania na vijana wa vyama vyote kuhakikisha wanamtafutia ushindi mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan.
Amesema vijana wanapaswa kujitokeza kumnadi Dk Samia kwani kampeni ya Banda la Mama inalenga kumpatia ushindi wa kati ya asilimia 80 hadi 100 kutokana na kazi kubwa na mafanikio aliyoyapata katika uongozi wake. SOMA: Samia asimamia miradi ya kimkakati
Maganza ameeleza kuwa kampeni hiyo haina mlengo wa kisiasa, bali ni jukwaa la kuonesha utambuzi wa wananchi kwa juhudi na maendeleo yaliyofanywa na Dk Samia katika kuimarisha ustawi wa Taifa. Ameongeza kuwa vijana wanapaswa kulipenda Taifa, kulinda amani na kutumia tarehe 29 kushiriki uchaguzi kwa amani, wakishindana kwa hoja na siyo vurugu, kwa kutambua kuwa Tanzania ni nchi yao