Barabara Kyema – Katerero yafikia asilimia 80

KAGERA: Mradi wa Barabara inayowaunganisha wananchi wa kata Katerero, Bujugo na Kasharu unaotelezwa na Wakala ya Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) kwa kiwango cha lami kilometa 0.55 chini ya mkandarasi Kashico LTD umefikia asilimia 80.

Meneja wa TARURA, Wilaya ya Bukoba, Emmanuel Yahana amesema mradi huo umetekeleza kigezo cha mwenge namba 2.2 cha mwenge wa uhuru na sera ya barabara na mradi ulianza kutekelezwa Agosti 16, 2024 ukitarajiwa kukamilika Oktoba 12, 2025 huu

Amesema mradi huo unazisaidia kata hizo kufuata huduma katika Halmashauri ya Bukoba huku akitaja uwepo wa ongezeko la majengo ya kibiashara katika eneo hilo na kupunguza changamoto ya wananchi kuzunguka kuzifikia kata hizo.

“Mradi huo umetekelezwa kwa awamu 4 na sasa tunaendelea vizuri ambapo sasa katika hatua zote za utekelezaji ni kumurahishia mwananchi kupata huduma na katika maeneo haya tumeanza kushuhudia ujenzi wa maduka na ongezeko la wakazi wakati zamani hata barabara ilikuwa haipitiki,” amesema Yohana.

Baadhi ya wananchi wa kata ya Katerero Halmashari ya Bukoba mkoani Kagera wameishukuru Serikali kwa kuwajengea mradi barabara hiyo kwani kwa sasa Hawana Hofu na vyombo vyao vya Usafiri.

Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 imeweka Jiwe la Msingi katikamradi huo ambao unaendeleaje kutekelezwa kwa viwango huku watumishi wa jengo jipya la halmashauri mpya a Wilaya ya Bukoba wakishuhudia lami hadi mlangoni kwao

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Ismail Ussi ameipongeza Tarura kwa usimamizi na utekekezaji barabara na kuwataka wananchi waendelee kutunza miundombinu ya barabara na kufanya uwekezaji kwani uwepo wa barabara unarahisisha mawasiliano.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button