Bayrou aondoka, Macron aanza mchakato kumtafuta mrithi

PARIS, UFARANSA: WAZIRI Mkuu wa Ufaransa, Francois Bayrou ameondolewa madarakani baada ya serikali yake kupoteza kura ya imani katika Bunge la Kitaifa. Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron anatarajiwa leo Jumanne kukubali kujiuzulu kwa Bayrou kufuatia hatua hiyo, ambayo imeibua tena mkwamo wa kisiasa nchini humo.
Taarifa zinasema Macron yupo mbioni kumteua Waziri Mkuu mpya, ambaye atakuwa wa saba katika kipindi cha utawala wake, ili kujaza nafasi hiyo na kuzuia kuzuka kwa mgogoro mpya wa kisiasa. Bayrou alipoteza kura ya imani aliyoitisha mwenyewe baada ya wabunge 364 kupiga kura ya kutokuwa na imani na serikali yake, huku 194 pekee wakipiga kura ya kuunga mkono.
Kwa mujibu wa Ikulu ya Ufaransa, Macron atakutana na Bayrou baadaye leo ili kuruhusu kujiuzulu kwake. SOMA: Uongozi wa Bayrou watingishwa



