Benki 35 kushiriki wiki huduma ya kifedha

BENKI 35 nchini zinatarajia kushiriki Maadhimisho ya 3 ya Wiki ya Huduma ya Fedha Kitaifa yanayoanza leo Arusha.

Lengo la maadhimisho hayo ni kutoa elimu kwa Wananchi kutumia huduma za kifedha kwani idadi ya watuamiji hairidhishi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamishina wa Idara ya Uendelezaji wa sekta ya fedha katika Wizara ya Fedha na Mipango,Dk Charles Mwamwaja alisema hadi sasa Wananchi asilimia 53.8 ndio wanatumia huduma ya kifedha.

Alisema hadi kufikia mwaka 2025 wanatarajia huduma ya kifedha kwa Wananchi ifikie asilimia 85 kote nchini ili uchumi wa nchini uweze kukuwa tofauti na ilivyo sasa.

Mwamaja alisema matarajio hayo yanaweza kufikiwa kwa kutoa elimu kwa wananchi faida ya kutumia huduma za kifedha,kutoa elimu ya usimamizi wa fedha binafsi katika utumiaji,kutoa elimu ya jinsi ya kuhifadhi akiba na kutoa elimu ya kujua haki ambayo anapata mwananchi akitumi huduma ya fedha .

Kamishina alisema kuwa huduma isiyokuwa rasmi kama vile kuhifadhi fedha ndani,kwenye magodoro ,vihenge,chini ya ardhi na sehemu nyingine zina hasara zake hivyo aliwataka wananchi kote nchini kufika katika katika viwanja vya Sheik Amri Abed kupata elimu ya utumiaji wa huduma ya fedha kwa maendeleo ya nchini.

Pamoja na kutoa elimu kwa Wananchi pia wameweka mikakati ya kutoa elimu katika ngazi ya shule za msingi na sekondari na ikiwezekana katika ngazi ya vyuo ili wanafunzi waweze kujua umuhimu wa kutumia huduma ya kifedha wakiwa wadogo tofauti na ilivyo hivi sasa.

Mwamaja alisema kuwa utamaduni huo ukijengwa katika ngazi hiyo ya chini uelewa unaweza kuwa mkubwa na faida kwa nchini kwani vijana wadogo wanaweza kutumia na kujua umuhimu wake wakiwa vijana.

Naye Meneja Msaidizi wa Mawasiliano wa Benki Kuu (BOT)  nchini, Noves Mosses alisema kuwa kauli mbiu ya wiki ya Maadhimisho ya Huduma ya Kifedha nchini ni ‘’elimu ya kifedha  msingi wa maendeleo ya kiuchumi.

Naye Grace Masambaji Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoani Arusha ametoa wito kwa wananchi mkoani Arusha kuhakikisha wanatembelea mabanda ya vyama vya ushirika kupata uelewa wa namna ya vyama hivyo vinavyofanya kazi.

Masambaji alisema kuwa Mkoa wa Arusha una vyama vitano vya ushirika na vinavyofanya kazi vizuri ikiwa ni pamoja na kutumia huduma za kifedha kwa wanachama wake hivyo wananachi wanapaswa kutembelea na kupata uelewa zaidi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button