Bibi matatani kilimo cha bangi

KATAVI; Watu watatu wamekamatwa na askari wa maliasili wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi kwa tuhuma za kujihusisha na kilimo haramu cha bangi ndani ya eneo la hifadhi ya misitu ya Kijiji cha Kapanga.
Watuhumiwa hao wawili ni wanaume na mmoja ni bibi mwenye umri wa miaka 65, lakini majina yao hayakutajwa kwa vile upelelezi unaendelea wa kutafuta watuhumiwa wengine, wanadaiwa kulima bangi kwenye eneo la takriban ekari tisa ndani ya misitu hiyo, ambayo inalindwa kwa ajili ya utekelezaji wa biashara ya kaboni.

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu, amelaani vikali vitendo hivyo, akisema ni kinyume na juhudi za uhifadhi wa mazingira na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya kaboni vijijini.
Amewataka wananchi wanaovamia maeneo ya misitu ya biashra ya kaboni, kuacha kulima bangi na kujihusisha zaidi ya kilimo cha mazao mengine yenye fursa za kiuchumi kama pamba, tumbaku na ufuta tena katika maeneo yaliyorasimishwa kwa ajili ya shughuli hizo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Ofisa Rasilimali Watu na Utawala Clavery Reginald, amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika itaendelea kufanya doria mbalimbali kwa maeneo yote ya misitu iliyotengwa kwa ajili ya biashara ya kaboni na maeneo yote ya uwekezaji ili kuilinda isiharibiwe na wenye nia ovu.




Google provides awesome remote work opportunities, allowing me to earn $2000-$3000 weekly with just 2-4 hours of daily work. It’s been a game-changer, offering flexibility and reliable income. If you’re seeking a genuine way to earn online, don’t miss this chance. Start today and transform your life!
.
More Details For Us →→ http://www.big.income9.com