SERIKALI imetoa Sh bilioni 14.4 kutelelezaji mradi wa ulipaji fidia, mradi wa magadi soda ya Engaruka uliopo wilayani Monduli mkoani Arusha.
Aidha wananchi 595 kutoka vijiji vinne vya Engaruka, Chini, Mbaash, Idonyonado na Irerendeni vitanufaika na fidia ya Sh bilioni 6.2 huku fedha zingine zilizobaki zikienda katika shughuli mbalimbali za miradi ya maendeleo.
Akizungumza wilayani hapo na wananchi wa eneo la Engaruka mkoani Arusha kuhusu ulipwaji wa fidia hiyo,Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Seleman Jafo amesema fedha hizo zimetolewa na Rais Samia Hassan Suluhu ikiwa ni mkakati wa kuendeleza miradi ya kimkakati yenye tija kwa taifa.
Amesema awali mradi huo ulikwama kutokana na changamoto za kimazingira katika Ziwa Natroni na siasa nyingi zilichelewesha mradi huo lakini serikali ikafanya utafiti tena na kuja na maamuzi kutoka kwa wataalam na kuona eneo la vijiji vinne linafaa sana katika uchimbaji magadi hayo ambalo ni eneo la uwanda wa juu wa ziwa hilo lenye magadi soda ya kutosha.
“Fedha zimeshaingizwa kwaaajili ya ulipaji fidia kupitia akaunti ya NDC huku fedha nyingine zitalipa fidia huku zilizobaki zitatengeneza miundombinu ya barabara, kituo cha afya na huduma nyingine za kijamii ”
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi , Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Haifa la Maendeleo (NDC) Dk Nicolaus Shombe amesema mradi huo wa magadi soda umechukua miaka 29 tangu ulipoanza mchakato wake na unahistoria kubwa kwani ulianza miaka kadhaa iliyopota lakini kunamambo ya kisiasa yaliingia na kupelekea kuchelewa kuanza.