Bil 4/- kujenga chuo cha afya Rombo

ARUSHA: SERIKALI imetoa Sh bilioni 4 kwa ajili ujenzi wa chuo cha afya kitakachojengwa muda wowote kuanzia sasa wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro.
Lengo ni kuzalisha wataalamu wabobezi katika sekta ya afya watakaohudumia jamii mbalimbali nchini
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dk Seif Shekalaghe ameyasema hayo jijini Arusha wakati wa makabidhiano ya hati ya miliki wa eneo katika Halmashauri ya Rombo yaliyofanyika katika Chuo cha Afya na Maendeleo ya Elimu na Afya Arusha (CEDHA).
Amesema hatua hiyo ni ahadi ya Makamu wa Rais, Dk, Philip Mpango aliyoitoa alipofika wilayani Rombo kwa ajili ya ufunguzi wa Hospitali ya Wilaya ambapo aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Profesa Adolf Mkenda aliomba kujengwa chuo hicho.
“Serikali kupitia Wizara ya Afya imeanza kutekeleza malekezo ya Dk Mpango na tayari Sh bilioni 4 zimetenga na hivi sasa michakato ya manunuzi tayari imeshaanza kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho kitakachowahudia wanachi lakini pia tumpongeza Profesa Mkenda kwa kutimiza wajibu wake kuhakikisha chuo hiki kinamalizika haraka na kuanza kutoa mafunzo,” amesema.
SOMA ZAIDI
Dk Shekalaghe ametoa rai kwa wananchi kuhakikisha wanatumia fursa ya chuo hicho kitakapomalizika kujengwa kwaajili ya kuwapeleka watoto kwaajili ya kupata elimu ikiwemo ulinzi wa miundombinu
Naye, Mkurugenzi wa Mafunzo na Maendeleo ya Rasilimali Watu katika Sekta ya Afya, Dk Saitore Laizer amesema tasnia ya mafunzo ya sekta ya afya nchini imepata historia nyingine kutokana na ujenzi wa chuo cha afya kitakachotoa programu zaidi ya tano zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 2,000
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
THIS→→→→ http://www.job40.media