Bil 51/- kukuza bunifu za kilimo kwa vijana

Shirika la AGRA Tanzania kwa Kushirikiana na Sahara Accelerator (Sa)kupitia mradi wa Youth Entrepreneurship for the future of food and Agriculture(YEFFA) wametoa kiasi cha Sh Bilioni 51.2 ili kufikia vijana 265,000 watakaojihusisha na masuala ya kilimo.
Akizungumza wakati wakijadili na vijana kuhusu fursa hiyo jijini Dar es Salaam,Adam Mbyallu kutoka kutoka Taasisi ya Sahara Accelerator amesema fursa hiyo inajumisha mnyororo wa thamani kwa mazao manne ambayo ni mbogamboga na matunda,alizeti,mpunga na mahindi.
“Tuna hakikisha namna gani tunaweza kusaidia upatikanaji wa vifaa vya kilimo kupitia teknolojia za kidigitali tunasaidia vijana wenye bunifu mbalimbali zinzojibu changamoto za upatikanaji wa vifaa za kilimo,”ameeleza Mbyallu.
Amesema kupitia bunifu hizo watawapatia vijana hao mafunzo,mentorship na kuwaunganisha wa wadau mbalimbali na kusaidia kwenda shambani kwenye kilimo na kujiuza.
Amefafanua kuwa bunifu wanazotafuta zitajibu changamoto za kilimo kama vifaa,mafundi,masoko,udhibiti wa mazao,uharibifu wa mazao baada ya mavuno changamoto ambazo wadau wa kilimo walisema zipo.
“Maeneo hayo yote kama vinavifaa vya kilimo vingesaidia sana vijana kujiajiri kwenye kilimo kama watajiajiri tunaangalia jinsi ya kuwawezesha kupitia teknolojia ya kidijitali.”

Mbyallu amesema ili kufanikisha upatikanaji wa bunifu hizo wamefungua dirisha la usajili wa bunifu kwa muda wa miezi miwili ambapo itafungwa Agosti 18,2025 na zitachunjwa kuangalia kama bunifu hizo zinakidhi vigezo na baada ya hapo watawaunga mkono.
“Tutawaunga mkono Kwa mafunzo,mentorship,changamoto na kuwaunganisha na wadau watakaowasaidia bunifu zao kwenda soko kama wadau wanaouza zana za kilimo,mafundi wa zana za kilimo,wanaotengeneza zana za kilimo,taasisi za fedha na wadau wengine,”amesisitiza
Ameongeza “Bunifu zitakwenda kwenye mazao manne yamegawiwa katika kanda kuna miradi kulingana na mazao ya eneo mfano Morogoro wanajikita na mbogamboga na alizeti ,Mbeya wana mbogamboga na mpunga ,Njombe Mbogamboga na Mahindi,Singida ni alizeti kila kanda imepewa aina ya zao tunakwenda kote.”



