Bodaboda Tanga hawataki maandamano

TANGA: CHAMA cha Madereva wa Bodaboda na Bajaji Mkoa wa Tanga (UWAPIBATA)kimewapiga marufuku wanachama wake kutoshiriki au kujihusisha na maandamano yanayotajwa kufanyika Desemba 9.
Akitoa tamko la makubalinao hayo kwa waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Chama cha Bodaboda, Tanga Mohamed Chande amesema kuwa iwapo madereva hao watabainika kushiriki hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Amesema kuwa iwapo mwanachama wao yoyote atashiriki kwenye tukio hilo atakuwa amejivua uwanachama hataruhusiwa kushiriki kwenye shughuli za biashara hiyo sambamba na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
“Nipende kuwaasa madereva wa bodaboda mkoani hapa tusikubali kushawishiwa kwa fedha au ulaghai na kushiriki kwenye kuvunja amani ya nchi yetu,kwani sisi tunajukumu la kulinda na kutunza amani kwa ustawi wa taifa letu,” amesema Chande
Kwa upande wake, Kamanda wa UWABIPATA, Hamis Ibrahim amesema kuwa tayari wameshawaini watu ambao sio waaminifu wanajipenyeza kwenye shughuli za bodaboda kwa lengo la kufanya ushawishi wa maandamano hayo.

“Sisi Tanga tupo macho viongozi wa mkoa na wilaya lengo ni kuhakikisha Tanga yetu inakuwa ni yenye amani na usalama ,na niwataka mtoe taarifa kwa viongozi na vyombo vua usalama iwapo utapakia abiria ambaye unamtilia mashaka,”amesema Ibrahim.



