BOT: Uchumi Tanzania kukua 7.2%

UCHUMI wa Tanzania Bara unatarajiwa kukua kwa asilimia sita katika robo ya kwanza ya mwaka 2026, huku uchumi wa Zanzibar ukitarajiwa kukua kwa asilimia 7.2 katika kipindi hicho.
Sambamba na matarajio hayo, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetangaza kuendelea kubakiza riba ya Benki Kuu (CBR) katika kiwango cha asilimia 5.75 kwa robo ya kwanza ya mwaka 2026. Uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha Kamati ya Sera ya Fedha (MPC) kilichofanywa Januari 7, 2026.
Gavana wa BoT, Emmanuel Tutuba alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akitangaza uamuzi huo wa Kamati ya MPC mbele ya wadau wa sekta ya fedha zikiwamo benki mbalimbali nchini na waandishi wa habari.
Tutuba alisema uchumi wa Tanzania Bara katika robo ya kwanza ya mwaka 2026, unatarajiwa kukua kwa asilimia sita huku uchumi wa Zanzibar ukitarajiwa kukua kwa asilimia 7.2. Tutuba alisema kamati hiyo ilibaini kuwa uchumi wa Tanzania Bara kwa mwaka 2025 uliendelea kukua kwa kasi ya kuridhisha ya asilimia 5.9 na ukuaji huo ulichangiwa zaidi na shughuli za kilimo, madini na ujenzi.
Aidha, kwa upande wa Zanzibar ukuaji wa uchumi wa mwaka 2026 unatarajiwa kuchangiwa zaidi na shughuli za ujenzi, utalii na uzalishaji viwandani. Gavana wa BoT alisema ili kuendelea kuimarisha shughuli za uchumi, Kamati ya MPC imeamua kuendelea kubakiza riba ya CBR kuwa asilimia 5.75 kama ilivyokuwa katika robo ya nne ya mwaka 2025.

Amesema uamuzi huo wa kubakiza riba hiyo umefikiwa kwa kuzingatia matarajio ya mfumuko wa bei kuendelea kuwa ndani ya lengo la asilimia tatu hadi tano. “Kubakiza riba hiyo kutasaidia kuendelea kuchagiza ukuaji wa shughuli za kiuchumi nchini na kuwezesha ukuaji wa uchumi kuwa wa kuridhisha,” alisema Tutuba.
Aidha, amesema uamuzi huo, BoT itatekeleza Sera ya Fedha kwa kuhakikisha riba ya mikopo ya siku saba baina ya benki inabaki ndani ya wigo wa asilimia 3.75 hadi 7.75. Pia, amesema BoT itaendelea kutekeleza sera za mikopo kwa sekta binafsi ambayo iliongezeka kwa wastani wa asilimia 20.3 kwa Tanzania Bara na Zanzibar.
Kuhusu mfumuko wa bei, Tutuba alisema unaendelea kubaki ndani ya lengo la asilimia tatu hadi tano. BoT imeeleza kuwa mfumuko wa bei uliendelea kuwa tulivu katika robo ya nne ya mwaka 2025, ambayo Tanzania Bara ulirekodi wastani wa asilimia 3.5, huku Zanzibar ukiwa asilimia 3.4.
Gavana Tutuba alisema mazingira mazuri ya uchumi wa dunia pamoja na utekelezaji madhubuti wa sera ya fedha yamechangia hali hiyo. Kwa upande wa uchumi wa dunia, Tutuba alisema uliendelea kuimarika mwaka 2025 licha ya changamoto za kisiasa na kibiashara. SOMA: Mwinyi aiomba UNESCO kusaidia uchumi wa Buluu Zanzibar
Amesema Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) lilikadiria uchumi wa dunia kukua kwa asilimia 3.2 mwaka 2025 na mwenendo huo unatarajiwa kuendelea mwaka huu. Aidha, alisema kupungua kwa bei za nishati kumeendelea kusaidia kupungua kwa mfumuko wa bei duniani.
Amebainisha kuwa bei ya mafuta ghafi ilipungua na kufikia kati ya Dola za Marekani 62 hadi 65 kwa pipa katika robo ya nne ya mwaka 2025, hali inayotarajiwa kuendelea kupunguza shinikizo la mfumuko wa bei na mahitaji ya fedha za kigeni nchini. Kuhusu bei ya dhahabu, Tutuba amesema imeendelea kuongezeka na kufikia Dola za Marekani 4,421.65 kwa wakia, hatua inayotarajiwa kuongeza mapato ya fedha za kigeni na kuimarisha thamani ya Shilingi.
Kuhusu akiba ya fedha za kigeni amesema iliendelea kuimarika na kufikia zaidi ya Dola za Marekani bilioni 6.3, kiasi kinachotosheleza uagizaji wa bidhaa na huduma kwa takribani miezi 4.9. Kuhusu thamani ya Shilingi, Tutuba alisema iliendelea kuwa tulivu, ikiongezeka kwa takribani asilimia 0.8 mwishoni mwa robo ya nne ya mwaka.




Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Jobathome1.Com
I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…
This is what I do………………………………….. https://Www.Cash54.Com
I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…
This is what I do………………………………….. https://Www.Payathome9.Com