CCM kujenga soko jipya Ilomba – Mwakisu

MBEYA : MGOMBEA Udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Ilomba jijini Mbeya, Nwaka Mwakisu, amewasihi wakazi wa kata hiyo kumpigia kura chama hicho kwenye uchaguzi wa Oktoba 29 mwaka huu.

Alisisitiza kwamba kura zao zitasaidia kuondoa changamoto zinazowakabili, ikiwemo ukosefu wa soko, vumbi na tope kutokana na ubovu wa barabara. SOMA: CCM kuimarisha kilimo biashara

Mwakisu aliahidi hayo wakati wa mkutano wa kampeni wa mgombea ubunge wa CCM katika jimbo la Uyole, Dk. Tulia Ackson, uliofanyika katika viwanja vya soko la Ituha lililopo Kata ya Ilomba. Alisema maendeleo ya kata yanahitaji ushirikiano wa wananchi na viongozi katika kuhakikisha miradi muhimu inatekelezwa.

Mgombea huyo ameeleza kuwa wakazi wa Ilomba ni wafanyakazi wa bidii katika kilimo na biashara, lakini wanakosa soko la kisasa la kuuza bidhaa zao. Hali hiyo inawapa changamoto kubwa za kifedha na kibiashara, hivyo umuhimu wa kuanzishwa kwa soko hilo.

Aidha, Mwakisu amesisitiza kuwa CCM ina historia ya kusaidia maendeleo ya wananchi kupitia miradi ya kijamii na miundombinu, na kwamba kura zao ni njia ya kuhakikisha changamoto za kero za kila siku zinatatuliwa.

Katika mkutano huo, wakazi walipata fursa ya kuuliza maswali na kutoa mapendekezo yao kuhusu miradi ya maendeleo. Mwakisu aliwahakikishia kuwa matakwa yao yatalindwa na kutekelezwa pale CCM itakaposhinda uchaguzi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button