CCM masikio Kamati Kuu leo uteuzi

DODOMA : CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) leo kinatarajiwa kuteua wanachama wa chama hicho walioomba kugombea ubunge na ujumbe wa baraza la wawakilishi wa jimbo na viti maalumu.
Ratiba ya CCM ya uteuzi wa wagombea wa nafasi za ubunge, uwakilishi, udiwani wa kata/wadi na viti maalumu kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu inaonesha leo Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa itakutana kufikiria na kuteua majina ya wana CCM wasiozidi watatu walioomba nafasi ya kugombea nafasi hizo ili wakapigiwe kura za maoni. Juzi Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan alisema Kamati ya Maadili ya CCM ingekutana jana kupitia majina ya wagombea.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Agosti 22, mwaka huu, Halmashuri Kuu ya chama hicho ya Taifa inatarajia kukaa kikao kufikiria na kufanya uteuzi wa mwisho wa majina ya wanachama wanaoomba nafasi ya ubunge na ujumbe wa Baraza la Wawakilishi wa jimbo na viti maalumu.
CCM imetangaza keshokutwa kutakuwa na mikutano mikuu maalumu ya mikoa ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kupiga kura ya maoni kwa wagombea wa ubunge wa viti maalumu (Tanzania Bara) na wagombea ubunge/uwakilishi wa viti maalumu (Zanzibar) vya mikoa.
Ratiba hiyo inaonesha kuanzia keshokutwa hadi Agosti 3, mwaka huu kutakuwa na mikutano ya kujitambulisha kwenye kata/ wadi na jimbo kwa wagombea wa ubunge, uwakilishi na udiwani kwa Zanzibar na Tanzania Bara.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo mikutano mikuu ya kata/ wadi na jimbo itafanyika Agosti 4, kupiga kura za maoni za wagombea wa ubunge, ujumbe wa baraza la wawakilishi na udiwani wa kata/wadi (kwa upande wa Zanzibar na Tanzania Bara). SOMA: Wajumbe CCM sasa ‘kufyeka’ wagombea Agosti 4
Ratiba inaonesha Agosti 5, kamati za siasa za kata/ wadi zitawajadili wagombea udiwani na kutoa mapendekezo yake kwa Kamati ya siasa ya jimbo/wilaya na Agosti 6, Kamati ya siasa ya jimbo itawajadili wagombea ubunge, uwakilishi na udiwani wa wadi kwa upande wa Zanzibar na kutoa mapendekezo yake kwa kamati ya siasa ya wilaya. Vikao vya kamati za siasa za wilaya kujadili wagombea ubunge, ujumbe wa baraza la wawakilishi na udiwani na kutoa mapendekezo yake



