CCM yajipanga mchakato katiba mpya

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimejipanga kuhakikisha mchakato wa katiba mpya unakamilika katika awamu ijayo ya uongozi, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha demokrasia na haki sawa kwa Watanzania wote.

Mgombea Mwenza wa Urais kupitia CCM, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, akihutubia mkutano wa kampeni katika Kata ya Dutwa, wilayani Bariadi mkoani Simiyu, alisema chama hicho kimekusudia kuendelea kujenga mazingira ya uwazi na ushirikishwaji wa wananchi katika maamuzi makubwa ya kitaifa.

“Katiba mpya ni moja ya mambo makubwa tuliyoyabeba. Tunataka kila Mtanzania ajivunie Katiba inayojibu mahitaji ya sasa. Aidha, tutaimarisha utawala wa sheria bila upendeleo; tajiri na maskini wote watapata haki sawa,” alisema.

Aliongeza kuwa pamoja na Katiba, CCM imejipanga kuendeleza amani na mshikamano wa taifa, akibainisha kuwa utafiti uliofanyika unaonyesha asilimia 90 ya wananchi wanatilia mkazo umuhimu wa amani na utulivu wa nchi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button