CHATO: Wagonjwa 1,082 Wafaidika na Huduma za MOI

CHATO : ZAIDI ya wagonjwa 1,082 wamefaidika na huduma za kibingwa na kibobezi za Mifupa, Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu zinazotolewa na Taasisi ya MOI katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Chato.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Balozi Dk. Mpoki Ulisubisya, wakati wa ziara yake katika hospitali hiyo. Dk. Mpoki amesema MOI itaendelea kusogeza huduma zake za kibingwa na kibobezi katika hospitali za kanda ili wananchi waweze kupata matibabu karibu na makazi yao.

“Taasisi ya MOI itaendelea kushirikiana na Hospitali ya Kanda ya Chato ili wagonjwa kutoka mkoa wa Geita wenye changamoto za mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu wahudumiwe hapa hapa bila kulazimika kusafiri hadi Dar es Salaam,” amesema Dk. Mpoki.

Ameongeza: “Hii itasaidia kupunguza gharama na usumbufu kwa wagonjwa ambao vinginevyo wangesafiri umbali mrefu kupata huduma zinazotolewa na MOI.” SOMA: Watumishi Moi wakumbushwa maadili, lugha za staha

Akimkaribisha Dk. Mpoki, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Kanda ya Chato, Dk. Oswald Lyapa, amesema idadi hiyo imerekodiwa kuanzia Novemba 2024 hadi Septemba 2025 na wagonjwa wengi kutoka kanda hiyo na mikoa jirani wanazidi kunufaika na kliniki hii.

Daktari kutoka Kitengo cha Mifupa, Dkt. Jackson Fulani, amefafanua kuwa kati ya wagonjwa 1,082, 722 walikuwa wagonjwa wa mifupa, huku 360 wakiwa ni wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu. MOI itaendelea kujenga uwezo wa hospitali za mikoa katika utoaji wa huduma za kibingwa za mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu ili kuhakikisha huduma hizo zinasogezwa karibu na wananchi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button