Chifu Mbwiyamundu ajiandaa kupiga kura

MBINGA, Ruvuma: MTAWALA wa Himaya ya Wamatengo, Joan Ngapomba maarufu kama Chifu Mbwiyamundu, amesema yupo tayari kushiriki kupiga kura na amewataka watu wa jamii yake pamoja na Watanzania kwa ujumla kusikiliza sera za wagombea kipindi hiki cha kampeni na kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29.
Amesema, anahisi fahari kwa namna sasa bosi wao Chifu Hangaya, Rais Samia Suluhu Hassan, anavyowapa nafasi machifu kushiriki shughuli za kijamii tofauti na ilivyokuwa awali.
Chifu Mbwiyamundu amesema hayo leo Septemba 21 Jimbo la Mbinga Mjini kushiriki kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dk. Samia, akiendelea na ziara zake mikoa mbalimbali nchini kuinadi Ilani ya CCM 2025-30 sambamba na kuomba kura kwa wananchi.



