China yakubali kuimarisha amani duniani
CHINA : WAZIRI wa Ulinzi wa China Dong Jun, amesema China itaimarisha ushirikiano wa kijeshi na nchi jirani, na kwamba mataifa makubwa yanapaswa kuwa mstari wa mbele kulinda usalama wa kimataifa.
Waziri huyo aliyasema hayo katika hotuba yake pana kwenye kongamano la kila mwaka la diplomasia ya kijeshi ya China mjini Beijing.
“Tuko tayari kuendelea kukuza mahusiano mazuri na mataifa makubwa kudumisha maendeleo thabiti ya uhusiano wa kijeshi ili kulinda utulivu wa kimkakati wa kimataifa,”
“Tuko tayari kuendelea kuimarisha uhusiano wa kijeshi na nchi Jirani na kuboresha pande zote kuaminiana na kulinda usalama wa kikanda, na kutanua uhusiano wa kijeshi na nchi zote.”Alimalizia.
Wawakilishi wa nchi 90 wakiwemo wa mashirika ya kimataifa walihudhuria kongamano hilo la siku tatu linalokamilika kesho Jumamosi. SOMA : Rais Samia kuanza ziara China
Ingawa baadhi ya nchi ziliwatuma mawaziri wa Ulinzi kwenye kongamano hilo, mataifa ya Magharibi yalituma maafisa wa ngazi za chini.