Chongolo aomba bandari kavu Makambako

NJOMBE; Mgombea Ubunge Jimbo la Makambako kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo, amemuomba Rais Samia kuwe na bandari kavu katika eneo la Makambako , kwani kutarahisisha shughuli za upokeaji na usafirishaji wa mizigo kwenda nchi jirani kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Zimbabwe na kuongeza mzunguko wa kiuchumi.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika Makambako kwa ajili ya kumnadi mgombea huy, alisema licha ya hatua kubwa zilizofikiwa katika sekta mbalimbali, bado zipo changamoto ambazo zinahitaji msukumo.
Pia alimuomba Rais kuridhia kuanzishwa kwa kituo cha kuhifadhi na kununua mahindi cha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kutokana na wingi wa mahindi katika eneo hilo.
Alisema hatua hiyo itasaidia wakulima kupata soko la uhakika na kuzuia unyonyaji wa walanguzi.
Chongolo alipendekeza kuanzishwa kwa kituo maalum cha mizigo ili kuimarisha biashara na kuweka Makambako kama kiunganishi kikuu cha usafirishaji kwa ukanda wa Nyanda za Juu Kusini na nchi jirani.
Pia aliomba mradi wa Umeme wa Upepo, ambapo aliomba kumpatia andiko kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi huo.