Chongolo: Nchimbi ni chaguo sahihi

NJOMBE : MGOMBEA Ubunge Jimbo la Makambako ambaye pia ni Katibu Mkuu wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amesema kitendio cha Rais Samia Suluhu Hassan kumchagua Balozi Dk Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza wa urais kimetokana na sifa kubwa alizonazo za kiuongozi, uzoefu wa kitaifa na kimataifa na historia yake ndefu ndani ya chama.

Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Njombe Mjini, Chongolo alisema CCM ni chama chenye utamaduni na utaratibu madhubuti wa kuzalisha viongozi, na Dk Nchimbi ni zao la mfumo huo. SOMA: Samia: Tunajiamini, sera zetu zinaaminika

Alifafanua kuwa Nchimbi alianza safari yake ya uongozi akiwa chipukizi, akapanda ngazi kupitia Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), akawa kiongozi wa jumuiya hiyo, kabla ya kupanda zaidi hadi ngazi za kitaifa serikalini.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button