CHP yamchagua Ozel kuwa kiongozi

UTURUKI: CHAMA kikuu cha upinzani nchini Uturuki, CHP, kimemchagua tena Ozgur Ozel kuwa kiongozi wake katika mkutano mkuu uliofanyika Jumapili, Septemba 21, 2025, licha ya kuwepo kwa changamoto za kisheria.
Kesi kadhaa zimefunguliwa dhidi ya chama hicho, ikiwemo inayotaka kubatilisha uchaguzi wa Ozel uliofanyika Novemba 2023 kwa madai ya wizi wa kura. Hata hivyo, kura 835 za wajumbe zimemhakikishia kuendelea kuongoza chama hicho.
Uchaguzi huo unakuja wakati wapinzani wa Rais Recep Tayyip Erdogan wakikabiliwa na kesi na kukamatwa, hatua ambazo wakosoaji wanasema zinatumika kisiasa kudhoofisha vyama vya upinzani nchini humo. SOMA: Tanzania, Uturuki kuimarisha biashara



