CUF yatangaza vipaumbele 13 Morogoro

MOROGORO : MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Morogoro Mjini kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Nyambi Athuman amesema endapo wananchi watamchangua kuwa mbunge wao atasimamia utekelezaji wa Ilani ya chama chake yenye maeneo 13 ya vipaumbele.

Maeneo hayo ya vipaumbele ni pamoja na uboreshaji wa huduma za afya, elimu, maji na miundombinu ambayo ni maono ya kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), ifikapo mwaka 2030. Mgombea wa ubunge huyo alisema hayo katika mkutano uzunduzi wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu uliofanyika eneo la Soko la Mawenzi, Manispaa ya Morogoro juzi.

Alisema CUF inaamini katika falsafa ya ‘Haki Sawa kwa Wote’ inahakikisha kila mwananchi anapata haki zake za kiuchumi, kijamii, mazingira bora na kipato cha msingi. Mgombea huyo alisema katika ilani hiyo imeelekeza kuboresha afya njema hususani kwa akina mama wajawazito na watoto kwa kupatiwa huduma bure, ustawi wa jamii, elimu bora kuanzia awali hadi chuo kikuu na jumuishi, kusimamia usawa wa kijinsia na haki za kundi maalumu.

Alisema endapo atachaguliwa atahakikisha anasimamia ilani hiyo ambayo imeelekeza hatua mbalimbali zikiwemo za kuboresha huduma ya maji safi na usafi wa mazingira. SOMA: Mgombea urais CUF: Pigeni kura, msisuse

Alitaja maeneo ya vipaumbele katika ilani hiyo ni kutokomeza umasikini kwa kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia vikundi vya uzalishaji mali, SACCOS na huduma jumuishi za kifedha. Pia, kupanua ajira nadhifu kupitia programu za kilimo, biashara ndogo za kazi na viwanda vidogo na kuanzisha mpango wa ruzuku ya huduma za msingi kwa familia masikini.

Alivitaja vipaumbele vingine ni kutokomeza njaa, kukuza kilimo endelevu hususani uboreshaji wa huduma za ugani, pembejeo za kisasa kwa wakulima, kuendeleza kilimo cha umwagiliaji maeneo ya mabonde, kuwezesha masoko ya uhakika ya mazao kwa wakulima kupitia ushirika na mifumo ya kidijiti.

Naye Mwenyekiti mstaafu wa CUF Wilaya ya Morogoro kichama, Abeid Mlapakolo akimtambulisha na kumdani mgombea huyo wa ubunge alisema suala la upigaji kura ni haki ya wananchi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button