DART wapata tiba foleni, vituo vya mwendokasi

DAR ES SALAAM: MTENDAJI Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Dk Athumani Kihamia amesema jumla ya mageti janja 360 yatafungwa katika vituo vyote vya mwendokasi ili kupunguza mkururo kwa wananchi kupata huduma.

Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam katika ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ofisi ya Rais TAMISEMI walipotembelea kukagua maendeleo ya miradi ya DART awamu ya kwanza, yapili na ya tatu ikiwa pamoja na kukagua shehena ya mizigo ya mageti janja yaliyowasili nchini na kuhifadhiwa katika Kituo cha Dart Gerezani, Kariakoo.

Soma pia https://habarileo.co.tz/nauli-mpya-mwendo-kasi-dar-kuanza-leo/

Kihamia amesema mageti hayo janja mapya yana uwezo wa kufanya kazi kwa miaka nane pasi na kufanyiwa huduma ya marekebisho ‘service’.

Amesema katika kuhakikisha ufanisi wa mageti hayo vituoni, kila kituo kitakuwa na umeme wa uhakika ikiwemo kufunga majenereta saidizi ‘backup generator’ pia kuvuna umeme wa jua.

Habari Zifananazo

Back to top button