Dawa asili kutibu wenye vipara yagundulika

ARUSHA; UNA tatizo la kipara? Au una changamoto ya kuota nywele? Basi usihuzunike kuna matumaini makubwa kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania(TAWIRI).

TAWIRI imetangaza kugundua dawa ya asili ya kuotesha nywele au kuzuia nywele kuota, dawa inayotokana na mmea uitwao Mporojo.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha kuhusu ugunduzi huo, Mkurugenzi wa Utafiti wa TAWIRI, Dk, Julius Keyyu, amesema taasisi hiyo imefanya utafiti kwa kipindi cha miaka 12 na hatimaye imepata dawa hiyo.

Amesema utafiti ulianza mwaka 2013 na kukamilika mwaka huu katika mimea inayotumika kwa tiba asili katika ukanda wa kaskazini mwa Tanzania katika Wilaya za Ngorongoro, Mbulu na Hanang kwa watu jamii ya Maasai, Hadzabe, Datoga na Iraqw.

Ameongeza kuwa utafiti huo umekwenda zaidi ya matumizi hayo na kugundua uwezo wa mmea huu kuotesha nywele au kuzuia nywele kutoka na tayari umepata hati miliki.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button