DC Arusha aonya madiwani wanaodai 10% kwa wazabuni

MKUU wa Wilaya ya Arusha, Felician Mutahengerwa amewataka madiwani wa jiji la Arusha kuacha mara moja kukwamisha miradi ya maendeleo kwa kulazimisha kupewa 10% kwa wazabuni wanaopewa kazi katika jiji.

DC Mutahengerwa amesema hayo katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Arusha na kusema anayo taarifa ya madiwani wenye tabia hiyo hivyo.

Amesema inasikisha kuona diwani analazimisha apewe asilimia hiyo kwa mzabuni wakati kila kata imepewa Sh milioni 28 kwa ajili ya maendeleo tangu septemba mwaka huu lakini hakuna kinachofanyika hadi sasa kisa asilimia 10.

Mkuu huyo amesema katika vikao vya kata vinavyohusisha watendaji wote wa kata na diwani (WDC) kuna malumbano ya kutosha namna ya kupata kampuni ya kufanya ujenzi wa maendeleo na hiyo yote inatokana na madiwani katika kata hizo kuja na kampuni mfuko ili apewe kazi hatua ambayo hakuna kinachofanyika na fedha hadi leo ziko katika akaunti.

Amesema na kutoa mfano katika Kata ya Olmot kuna mwanasiasa wa CCM alikuja na hoja kwa kuwa kata hiyo kuna uwanja wa kisasa unajengwa kwa ajili ya AFCON hivyo ni lazima hazanati ya kisasa inapaswa kujengwa na hoja yake ilikubalika na serikali ilipelekea Sh milioni 450.

Mkuu huyo amesema toka zimepelekwa fedha hizo hadi sasa zaidi ya miezi mitatu hakuna kinachofanyika kwa kuwa watu wametanguliza maslahi binafsi na mradi huo umekwa kwani vikao vya WDC vikifanyika ni malumbano yasiyokuwa na tija .

‘’Nimesema madiwani acheni hiyo tabia ya kukwamisha miradi ya maendeleo na ninayo majina ya madiwani wenye tabia hiyo kwani haileti afya na picha kwa Jiji la Arusha’’alisema Mutahengerwwa

Mbali ya hilo Mkuu huyo wa wilaya alisikitishwa na ujenzi holela unaofanywa katika maeneo mbalimbali ndani ya halmashauri ya jiji la usiozingatia sheria na taratibu na wengi wao hawana vibali kutoka Idara ya Mipango Jiji na Idara ya Ujenzi.

Akizungumzia maeneo ya wazi ambayo Arusha ilibomoa nyumba kama vile eneo la wazi CCM mkoa, kaloleni ,fire na Kilombero kutafuta wawekezaji ili maeneo hayo yaendelezwe na ikishindikana yeye atawasiliana na serikali Kuu kuhakikisha mwekezaji yanaendeleza maeneo hayo.

Mkuu huyo amesema jiji ilibomoa maeneo hayo miaka miaka mingi iliyopita lakini hadi leo hakujaendelezwa na hajui kwa nini mwekezaji hajapatikana hivyo ni wakati wa Jiji kuendeleza maeneo hayo vinginevyo yeye ataomba msaasa serikali kuu ili maeneo yote yaendelezwe.

Amesema serikali inatafuta wawekezaji wa ndani na nje kuendeleza maeneo ili iweze kuingiza mapato lakini uongozi wa jiji la Arusha umekalia maeneo hayo na hakuna mpango wowote wa kuendeleza hiyo haivumiliki.

Akizungumzia kauli ya Mkuu wa Wilaya, Mstahiki Meya wa jiji la Arusha ,Maxmilian Iraghe amesema jiji la Arusha linafanya shughuli zake kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa na kamwe haliwezi kufanya shughu kinyume na taratibu kama inavyofikiriwa.

Habari Zifananazo

Back to top button