Dc Nzega aanza kusikiliza kero za wananchi

MKUU wa Wilaya ya Nzega, Naitapwaki Tukai ameanza ziara ya kusikiliza kero za wananchi kuanzia Aprili 3 hadi Aprili 9, 2025.

Ziara hiyo inayojulikana kama “Mtaa kwa Mtaa”, inalenga kufikia maeneo mbalimbali katika Kata ya Nzega Mjini Magharibi kujadili masuala ya maendeleo na mwendendo wa utoaji wa huduma za serikali.

Tukai, anatarajiwa kutembelea maeneo sita ambapo atakutana na wakazi wa eneo hilo kwa lengo la kusikiliza na utatua changamoto zao, na kutathmini miradi ya maendeleo inayotekelezwa.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Nzega imebainisha kuwa maenedo yatakayotembelewa ni pamoja na Ushirika (Shule ya Msingi Ushirika), mtaa wa Ipillii (Shule ya Msingi Ipillii), ofisi ya mtaa wa majengo pamoja na ule wa Mbugani. Maeneo mengine atakapozuru Mkuu huyo wa Wilaya ni mtaa wa Humbi ambapo atafanya mkutano na wakazi wa mtaa huo kwenye Ukumbi wa Serena.

“Ziara hiyo itahitimishwa Aprili kwa Mkuu wa Wilaya kutembelea na kukutana na wakazi wa mtaa wa Utemini  katika ofisi ya Serikali ya Mtaa huo,” imenkuliwa tarifa hiyo iliyosambazwa kwenye Mbao za matangazo na mitandao ya kijami.

Ziara hiyo inakuja huku pamoja na mambo mengine, Tukai amekuwa kiungana na juhudi za Rais wa Tanzania  kusisistiza utekelezaji wa  maendeleo ya ujenzi wa  miundombinu, vituo vya afya, na ujenzi wa shule kwa ajili ya kurahisisha upatikanaji wa huduma za elimu kwa wakazi wa Mji wa Nzega.

“Kwa kukutana moja kwa moja na wananchi, Mkuu wa Wilaya anatekeleza ajenda ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya utawala jumuishi unaowashirikisha wananchi katika ngazi za maamuzi,” aliisema Ofisa  Tarafa wa Tarafa ya Nyasa  Ricardo Katambi Komanya

Komanya alongeza kuwa Kaulimbiu ya ziara hii, #MtaakwaMtaa inasisitiza dhamira ya serikali kupeleka huduma karibu zaidi na wananchi ili kuhakikisha kila mmoja anashiriki kikamilifu katika safari ya maendeleo ya kata ya Nzega magharibu na Wilaya ya Nzega kwa ujumla.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button