DED Kondoa Mji aipa nguvu timu ya halmashauri

TANGA: Mkurugenzi wa Halimashauri ya Mji Kondoa Said Majaliwa ametembelea timu ya halimashauri hiyo inayoshiriki mashindano ya Shirikisho la Michezo Serikali za Mitaa Tanzania (SHIMISEMITA 2025) jijini Tanga na kuwataka wacheze kwa juhudi na maarifa ili waweze kurudi na ushindi.

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na wachezaji hao waliokuwa kambini kwa ajili ya kushiriki kwenye michezo hiyo ambayo inaendelea kutimua vumbi jijini Tanga ambapo amesema kuwa yupo kwa ajili ya kuwaongezea hamasa wachezaji hao.

“Niwahakikishie mimi kama Mkurugenzi nitaendelea kuwaunga mkono katika michezo kwani michezo huimarisha afya ,umoja na kudumisha amani miongoni mwetu na hivyo kuleta ari ya kufanyakazi,” amesema DED Majaliwa.

Michezo ya SHIMISEMITA imeanza rasmi Agosti 16 katika viwanja mbalimbali jijini Tanga na inatarajiwa kufikia tamati mnamo Agosti 29 mwaka huu.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button