Dhamira ya Nyerere na chimbuko la Azimio la Arusha

“HISTORIA ya Tanzania haiwezi kukamilika bila kutambua mchango wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere katika azma yake ya kuanzisha, kuliishi na kulipigania Azimio la Arusha.”
Mhifadhi Historia wa Makumbusho ya Azimio la Arusha, Elton Mjun anasema katika mazungumzo na gazeti HabariLEO yalipo makumbusho hayo jijini Arusha kuelekea maadhimisho ya miaka 26 tangu kifo cha mwasisi huyo wa taifa, kilichotokea Oktoba 14, 1999.
Mjun anasema Februari 5, 1967, Nyerere alianzisha Azimio la Arusha alipolihutubia taifa jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Mnazi Mmoja baada ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Tanganyika African National Union (TANU) cha Januari 26 hadi 28 mwaka 1967 kilichohudhuriwa na wajumbe 68 kutoka mikoa yote ya Tanzania.
Anasema kikao hicho kilitanguliwa na Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Tanu uliofanyika katika Ofisi za chama Mkoa wa Arusha mwaka 1967. Mjun anasema Nyerere na viongozi wenzake wakiwa katika mkutano huo walifikia uamuzi wa kukaa kikao kile kilichofanyika katika Jengo la Maendeleo ya Jamii Kaloleni ambacho kimsingi ndicho chimbuko la Azimio la Arusha.
“Katika kikao hiki ambacho Mwalimu Nyerere alikuwa Mwenyekiti, Rashid Kawawa Makamu Mwenyekiti na Oscar Kambona Katibu Mkuu wa Tanu sambamba na wajumbe wengine 68, walikubaliana kuanzishwa kwa Azimio la Arusha mwaka 1967,” anasema.
“Tunapoadhimisha miaka 26 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, huwezi kutenganisha historia ya Tanzania na Mwalimu Nyerere na huwezi kumtenganisha Nyerere na Azimio la Arusha,” anafafanua Mjun.
Anasema Nyerere alilitumia Azimio la Arusha kujenga Tanzania mpya, kwa kuhamasisha matumizi ya lugha ya Kiswahili kama lugha ya taifa, kuanzisha vijiji vya ujamaa, kujenga uadilifu kwa viongozi na watumishi wa umma na kujenga umoja wa kitaifa kwa kupiga vita ubaguzi wa kikabila, udini na hata ubaguzi wa rangi.
Kwa mujibu wa Mjun, wakati taifa linaadhimisha miaka 26 ya kifo cha Nyerere, Watanzania wanapaswa kutambua kuwa Makumbusho ya Azimio la Arusha ni moja ya zao la juhudi za Baba wa Taifa. “Watanzania wanapaswa kuyatumia makumbusho haya kujua historia yao kwa ufasaha hususani uanzishwaji na malengo ya Sera ya Ujamaa na Kujitegemea,” anasema.
Anaongeza: “…Na kupitia makumbusho haya ambayo Mwalimu Nyerere aliyaanzisha, Watanzania wanaweza kuyatumia kama nyenzo ya kujitathmini walipokosea jana, wanalopaswa kujifunza leo na kupata mwelekeo mpya na chanya kama taifa.
“Huwezi kuwa Mtanzania mzalendo na bora kama hujui historia yako vizuri, hivyo tunapoadhimisha miaka 26 ya kifo cha Baba wa Taifa, Watanzania wayaone na kuyatumia makumbusho haya kama moja ya nyenzo zinazoweza kuboresha maisha yao kwa kuwa Mwalimu Nyerere alipiga vita rushwa, ubadhirifu na uvivu.”
Anasema baada ya kuanzishwa kwa Azimio la Arusha mwaka 1967, wananchi waliliunga mkono na wakati huo pia yalianzishwa matembezi ya kuunga mkono Azimio la Arusha. Mjun anasema Nyerere aligundua kuwa licha ya wananchi kuunga mkono Azimio la Arusha, wengi wao walikuwa hawajaelewa vizuri madhumuni yake.
Kwa msingi huo anasema, mwaka huohuo 1967, Nyerere aliongoza matembezi ya kuvunja dhana kutoka kuwa
kwenye akili na kuwataka Watanzania walione Azimio la Arusha kuwa ni jambo linalopaswa kutoka moyoni.
Anasema Nyerere aliongoza matembezi ya kuunga mkono Azimio la Arusha kutoka Butiama hadi Mwanza, umbali wa takribani maili 133, hali iliyowafanya baadhi ya watu kuugua na wengine kuumia.
Kwa mujibu wa Mjun, kwa kutumia hali hiyo ya maumivu waliyoyapata, Nyerere aliwaeleza kuwa, maumivu ya mwili waliyoyapata wanapaswa kuyahamishia moyoni katika kutekeleza Sera ya Ujamaa na Kujitegemea kutoka katika vilindi vya mioyo yao na si kutembea kwa kuchosha tu mwili.
“Taifa linapoadhimisha kumbukumbu ya miaka 26 tangu Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere afariki dunia mwaka 1999,” anasema mwitikio wa Watanzania kutembelea Makumbusho ya Azimio la Arusha si mkubwa ikilinganishwa na wageni kutoka nje.
“Kwa wastani, kwa mwezi tunapokea wageni kati ya 300 hadi 400 wanaotembelea Makumbusho haya na miongoni mwao, Watanzania watu wazima wanaweza kuwa 50, wageni kutoka nje ya nchi 100 na waliobaki ni wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wanaokuja kujifunza,” anabainisha.
Kutokana na mwitikio huo mdogo wa Watanzania kujifunza vyema historia ya Azimio la Arusha na kujua vyema dhamira ya Baba wa Taifa kuanzisha makumbusho haya mwaka 1977, Mjun anahimiza Watanzania kufika hapo kwa wingi ili waone na kujua nchi yao imetoka wapi, wanapaswa kuwa viongozi wa namna gani, kuwa na Tanzania ya namna gani na utamaduni wa namna gani.
Anasema watumishi wa Makumbusho ya Azimio la Arusha wanafanya kazi kila siku kuanzia Jumatatu hadi Jumapili, hivyo ni fursa ya Watanzania kuyatembelea makumbusho hayo yanayopatikana kila siku katika siku saba za wiki.
Mjun anasema gharama za kutembelea Makumbusho ya Azimio la Arusha ni nafuu kwa kuwa Mtanzania mtu mzima anapaswa kulipa Sh 2,500, wanafunzi kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha sita Sh 1,000 na watoto chini ya miaka mitano ni bure.
Anasema baadhi ya wanafunzi wa vyuo wanaosomea masuala ya utalii na historia wamekuwa wakiyatumia
makumbusho hayo kwa mafunzo ya vitendo kwenye sekta ya utalii wa historia. Kwa sasa Makumbusho ya Azimio la Arusha yametimiza miaka 48 tangu yalipoanzishwa Februari 5, 1977 katika Mtaa wa Kaloleni, Arusha.




Make money while staying at home and working online. I just received $23,783 for my work last month, and I was doing this part-time. This year, I plan to earn even more, and I believe you can also make extra cash from this job. To join right now, follow the details on this website.
Open This… http://Www.Work99.Site
I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com