Diwani CCM auwa kwa panga

DIWANI wa kata ya Kiziguzigu wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma Martin Runaku Mpemba amekufa baada ya kupigwa mapanga na mtu asiyejulikana na kupelekea kifo chake.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kigoma, Christopher Palangyo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuitaka serikali kufanya iwezekanavyo ili waliohusika na tukio hilo wakamatwe.
Pallangyo alisema kuwa Marehemu alikutwa na maafa hayo April tatu mwaka huu majira ya usiku akiwa anarejea nyumbani kwake katika kijiji cha Kabingo ambapo alishambuliwa na kitu chenye ncha kali kichwani kilichosababisha kifo chake.

kizungumza na viongozi wa chama na waombolezaji mjini Kakonko amesema CCM imesikitishwa na tukio la kifo cha Diwani Mpemba na kwamba wananchi wawe na utulivu wakati huu ambao wanalitaka jeshi la polisi kuchukua hatua ili wahusika wakamatwe.
Palangyo ambaye amewasilisha salam za pole za Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu wa CCM Dkt Emmanuel Nchimbi kufuatia msiba huo, amesema Chama kinaungana na familia, wanaccm na wananchi wote katika msiba huo.
Kamanda wa polisi mkoa Kigoma,Filemon Makungu amekiri kuwepo kwa taarifa hizo na kwamba polisi itatoa taarifa baadaye kuhusu tukio hilo.



