Dk Bashiru, Ng’wasi waanza ziara Moro

MOROGORO: Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Balozi Dk Bashiru Ally, na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Ng’wasi Damas, wameanza ziara ya kikazi mkoani Morogoro kukagua maendeleo ya sekta za mifugo na uvuvi na kusikiliza changamoto zinazowakabili wadau wa sekta hiyo.
Viongozi hao wanatarajiwa kutembelea miradi mbalimbali ya ufugaji wa kisasa, vituo vya utafiti, masoko ya mifugo, maeneo ya ufugaji wa samaki, pamoja na miradi ya uvuvi iliyoanzishwa na serikali pamoja na sekta binafsi.

Aidha, wataonana na wafugaji, wavuvi na viongozi wa serikali za mitaa ili kupata taarifa za utekelezaji wa mipango ya serikali na kujadili namna bora ya kuongeza tija kwenye uzalishaji.
Akizungumza kabla ya kuanza kwa ziara hiyo, Waziri Dk Kakurwa amesema serikali imejipanga kuimarisha mifumo ya uzalishaji na kuongeza thamani ya mazao ya mifugo na uvuvi ili kuchangia kwa kiasi kikubwa kwenye pato la taifa.

Aidha, ameeleza kuwa ziara hiyo itasaidia kuchochea suluhisho la changamoto za muda mrefu kama upatikanaji wa pembejeo, masoko, miundombinu duni na vitisho kwa rasilimali za uvuvi.
Ziara hiyo inatarajiwa kutoa mapendekezo na maelekezo yatakayoboreshwa kwenye sera, mifumo ya usimamizi na uendelevu wa rasilimali za mifugo na uvuvi nchini.




