Dk Gwajima atembelea chuo kinachofundisha Kiswahili Namibia

NAMIBIA; Waziri wa Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk. Dorothy Gwajima ametembelea Chuo cha Triumphant kilichopo Windhoek, Namibia ambacho kinafundisha lugha ya Kiswahili kwa kwa kushirikiana na Baraza la Kiswahili la Taifa (Bakita).

Waziri Dk Gwajima aliambatana na Mama Anna Mkapa, ambate ni mjane wa Rais wa Awamu ya Tatu wa Tanzania, hayati Benjamin Mkapa. Pia waliambatana na Balozi wa Tanzania nchini humo, Caesar C. Waitara.

Akiwa chuoni hapo Dk Gwajima aliwahuhutubia wanafunzi hao pamoja kushuhudia shughuli mbalimbali zilizokuwa wakizifanya kwa kwa lugha ya Kiswahili, ikiwemo utumbuzaji wa nyimbo kwa lugha za Kiswahili.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button