Dk Mpango azindua hatifungani ya kijani miundombinuu ya maji

TANGA: Makamu wa Rais Dk Philip Mpango amezindua rasmi hatifungani ya kijani ya Mamlaka ya maji Tanga yenye thamani ya Sh bilioni 53.
Amesema kuwa hatifungani hiyo ni ya kihistoria kwakua itasaidia kuboresha huduma za maji huku wananchi wakipata faida kutokana na uwekezaji huo.
Aidha ameiagiza Mamlaka ya masoko na mitaji kuweka utaratibu wa mifumo ya tahadhari ili kufuatilia vihatarishi vinavyoweza kujitokeza kwenye utekelezaji wa hatifungani.
Pia amewataka wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ikiwemo sekta binafsi kushiriki katika ununuzi wa hatifungani hizo ili waweze kushiriki kwa vitendo kuunga mkono nia ya serikali kuwaletea maendeleo wananchi.