Dk Mwigulu aagiza mkandarasi kukamatwa, kuzuia hati yake

WAZIRI Mkuu Dk Mwigulu Nchemba, ameelekeza Jeshi la Polisi na Uhamiaji kuhakikisha wanamkamata na kuzuia hati ya kusafiria ya mkandarasi anayejenga mradi wa Kituo cha ukaguzi cha Pamoja kilichopo Muhalala mkoani Singida.

Dk Mwigulu amesema kuwa mkandarasi huyo aliaminiwa na Serikali kwa kupewa ujenzi wa mradi huo wa kimkakati uliosimama kwa zaidi ya miaka nane tangu mwaka 2016.

Mradi huo unaojengwa na kampuni ya Impresa di Costruzioni Ing. E. Mantovani S.p.A ulipaswa kukamilika mwaka 2018.

Ametoa agizo hilo leo Novemba 21, 2025 wakati alipokagua mradi huo katika ziara yake ya kikazi mkoani Singida ambapo atakagua miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi.

Dk Mwigulu amesema kuwa jitihada zimefanyika za kuona mradi huo unaendelea lakini mkandarasi amekuwa akileta ugumu katika utekelezaji.

“Mkandarasi huyu alitangazwa amefilisika na hawezi kuendelea na mradi na alielekezwa ailipe fidia Tanzania kwasababu ameicheleweshea mradi”

“Naelekeza, Kamishna wa uhamiaji kamata hati yake ya kusafiria, asitoke nje ya nchi mpaka jambo hili liishe, hii ni hujuma ya waziwazi, hii ni dharau ya waziwazi anaifanyia nchi yetu, Jeshi la Polisi mtafuteni mkandarasi huyu popote alipo, tumemuajiri, tunamlipa lakini anajiamulia Kama aendelee na kazi au asiendelee, huyu ni mhalifu akamatwe mpaka jambo hili liishe,” amesisitiza Dk Mwigulu

Dk Mwigulu amesema kuwa wakandarasi wa nje wanapaswa kufahamu kuwa wanapokuja kufanya kazi hapa nchini, watambue Tanzania imewaajiri na wasijione kama wao ni mabosi.

“Ninaelekeza wale washirika wetu katika mradi huu, ndani ya mwezi huu jambo hili liwe limekwisha watuambie wanaendelea ama hawaendelei, na kama hawataendelea Waziri wa Ujenzi uwapatie wakandarasi wadogo wamalizie kazi hii, hii nchi ni yetu na tunawajibu wa kuilinda, na Mheshimiwa Rais Dk Samia ametuambia hatuna mjomba, tuna mama tu anaitwa Tanzania.”

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Nowadays earning money online is very easy . Eanrs every month online more than $17k by doing very easy home based job in part time u can also do this simple online Job by visiting website
    More Details For Us→→ http://www.job40.media

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button