Mwinyi ahimiza kuendeleza maombi ya amani

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewahimiza wananchi kuendeleza utamaduni wa kuiombea nchi amani, ili mipango na miradi ya maendeleo iweze kutekelezwa kwa mafanikio. SOMA: TEF yawasihi Watanzania kuimarisha umoja, amani

Alhaj Dk. Mwinyi alitoa wito huo alipojumuika na waumini wa dini ya Kiislamu katika Sala ya Ijumaa iliyofanyika Msikiti wa Ijumaa, Malindi. Amesema kuwa baada ya kufanikisha Uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu, ni wajibu wa kumshukuru Mwenyezi Mungu na kuendelea kumuomba ili amani hiyo iendelee kudumu nchini.

Aidha, Dk. Mwinyi amefafanua kuwa kazi nzuri iliyofanyika kabla na wakati wa uchaguzi katika kuiombea nchi amani, inapaswa kuendelezwa kwa bidii na umoja zaidi. Ameeleza kuwa ni neema kubwa kwa taifa kubaki na umoja, amani, utulivu na mshikamano baada ya uchaguzi, na akasisitiza viongozi wa dini pamoja na waumini kuendelea kuiombea nchi ibaki salama wakati wote.

Habari Zifananazo

14 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button