Dk. Mwinyi asifu mafanikio ya uchumi shirikishi

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema mageuzi ya uchumi na fedha yaliyotekelezwa na Serikali yamekuwa msingi imara wa kuijenga Zanzibar shirikishi na yenye ustawi wa wananchi wote.
Akizungumza katika hafla maalum ya kumpongeza kwa mageuzi ya uchumi na fedha, utoaji wa gawio kwa wawekezaji wa Zanzibar Sukuk, na uzinduzi wa Skimu ya Hifadhi ya Jamii ya Kiislamu, hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Ikulu Zanzibar, Dk. Mwinyi amesema Serikali imepiga hatua kubwa katika kuimarisha uchumi wa taifa na kuboresha maisha ya wananchi.
Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa mafanikio hayo yametokana na sera madhubuti za kifedha, usimamizi bora wa fedha za umma, na matumizi ya teknolojia za kisasa, hali iliyochochea ukuaji wa uchumi kwa asilimia 7.2 na ongezeko la uwekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Alifafanua kuwa ndani ya kipindi cha miaka mitano, mapato ya Serikali yameongezeka kwa asilimia 278, huku mfumuko wa bei ukidhibitiwa kwa tarakimu moja. Aidha, sekta za utalii, kilimo na uvuvi zimeendelea kukua na kuimarika kwa kasi, zikichangia kwa kiasi kikubwa katika pato la taifa.
Rais Dk. Mwinyi alieleza kuwa hatua ya kutoa gawio la kwanza kwa wawekezaji wa Zanzibar Sukuk, tangu kuanzishwa mwaka 2024, ni ishara ya wazi ya dhamira ya Serikali kusimamia vyema dhamana zake za kifedha. Kupitia mpango wa Sukuk, Serikali imeweza kugharamia miradi mikubwa ya kimkakati, kuimarisha imani kwa wawekezaji na kufungua milango kwa sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa.
Alisisitiza kuwa mageuzi hayo yametekelezwa chini ya misingi ya uwazi, uwajibikaji na uadilifu, huku Zanzibar ikiweka historia mpya katika utekelezaji wa mifumo ya kifedha inayoendana na kanuni za Kiislamu. Aidha, Rais Dk. Mwinyi alisema Serikali imeanzisha mfumo wa bima ya Kiislamu kupitia Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC), utakaotoa huduma zinazofuata misingi ya sheria za Kiislamu.
Aliongeza kuwa mageuzi katika mifuko ya hifadhi ya jamii yameboresha ulipaji wa pensheni kwa wakati, usimamizi wa michango, na kuongeza faida kwa wanachama. SOMA: Rais Mwinyi : Kampeni za CCM zinaonesha taswira ya ushindi
Kupitia mifumo ya kidijitali, Serikali inalenga kuhakikisha kila mfanyakazi wa umma na sekta binafsi anasajiliwa na kulindwa dhidi ya changamoto za kiuchumi, maradhi, ajali na uzee hatua itakayojenga Zanzibar yenye haki, usawa na ustawi wa jamii.
I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com