Dk Mwinyi, viongozi wa nje wahudhuria misa kumuombea Mkapa

MTWARA: MISA takatifu ya kumbukizi ya miaka mitano ya kifo cha Rais wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin William Mkapa imefanyika leo katika kijiji cha Lupaso wilayani Masasi mkoani Mtwara.

Misa hiyo imeongozwa na Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ambapo amesema wanapomkumbuka mpendwa wao huyo wapeleke dua na sala zao ili Mwenyezi Mungu kama kuna makosa yoyote kwa mpendwa wao amuinue.

Pia imehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi akiwemo Msumbiji, Uganda, Marekani na zingine huku mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Hassan Mwinyi kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Askofu Mkuu huyo amesema kifo ni hatua kutoka katika mazingira kama wanayoishi wao hadi  leo hii imefikia miaka hiyo mitano tangu kifo cha mpendwa wao, siyo kwamba amemalizika bali ametoka katika maisha yao na kwenda kwenye maisha ya Mbinguni.

“Kifo siyo mwisho japo kuwa ni miaka mitano tangu kufariki bado anayo mengi ya kuwafundisha kutoka kwake na aliweza kutufundisha undani wa wazi kabisa wa yale ambayo ni ya kibinadamu yenye kumpendeza Mungu,”amesema Pengo

Mbali na hilo amezungumzia suala la jamii kuzingatia na kuendeleza maadili ambayo yalifundishwa na Benjamin William Mkapa ikiwemo yale yenye misingi ya kumpendeza Mungu.

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Msumbiji, Filipe Jacinto Nyusi amesema uongozi wa hayati Benjamin William Mkapa ulikuwa ni wa muelekeo mzuri kielimu
na katika hotuba zake alisisitiza suala la maendeleo lakini kuimarisha uhusiano, undugu baina ya Tanzania na Msumbiji,”amesema Nyusi

Kwa Upande wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amewataka watanzania kumuenzi Mzee Mkapa kwa kuendelea kudumisha tunu ya amani aliyonayo kwasababu ndio msingi wa maendeleo ya nchi na ustawi mkubwa wa wananchi.

Pia katika kipindi hiki ambacho watanzania wanaelekea kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025, amewaomba viongozi wa dini, wanasiasa na wengine waendelee kuhubiri amani ili waweze kushiriki uchaguzi huo katika hali ya amani na utulivu.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button