Dk. Nchimbi aahidi kukarabati barabara 16 Kilolo

IRINGA : MGOMBEA Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi amesema dhamira ya Chama Cha Mapinduzi endapo kitapewa ridhaa ya kuongoza miaka mitano ijayo ni kujenga na kukarabati jumla ya barabara 16 za Wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa mpira wa Isele, Ilula jimbo la Kilolo, Dk. Nchimbi alisema mpango huo umezingatia kilio cha wabunge na madiwani wa CCM waliopigania kwa muda mrefu suala la upatikanaji wa miundombinu bora ya barabara.

“Kupitia Ilani ya CCM tumeweka wazi dhamira ya kuhakikisha barabara muhimu zinaboreshwa. Baadhi zitajengwa kwa kiwango cha changarawe, nyingine kwa zege, na barabara tano zitajengwa kwa kiwango cha lami ili kufungua zaidi fursa za wananchi wa Kilolo,” alisema Nchimbi.

Aliongeza kuwa barabara hizo ni kiungo muhimu cha maendeleo ya wananchi, kwani zitasaidia kufanikisha shughuli za kiuchumi, usafirishaji wa mazao ya kilimo na kuongeza thamani ya maisha ya kila familia katika wilaya hiyo.

Wananchi waliohudhuria mkutano huo walimpongeza kwa mpango huo wakisema unagusa moja kwa moja changamoto kubwa wanazokutana nazo kila siku, hasa usafirishaji wa mazao kutoka mashambani kwenda sokoni. SOMA: CCM yaongoza kwa uzoefu-Dk.Nchimbi

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button