Dk Nchimbi: CCM imefanya makubwa

MWANZA; MGOMBEA mwenza wa urais kupitia CCM, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, amewashangaza wanaodai kuwa chama hicho hakijafanya lolote, akibainisha mafanikio makubwa yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Akihutubia wananchi wa Kwimba, Mwanza, Dk. Nchimbi amesema serikali ya awamu ya sita imejenga Hospitali ya Wilaya ya Kwimba, kuongeza vituo vya afya kutoka 50 hadi 61, shule za sekondari kutoka 34 hadi 43 na vijiji vilivyo na umeme kutoka 60 hadi 119.

Alisisitiza kuwa serikali ijayo ya CCM itaendeleza kasi hiyo kwa kujenga zahanati mpya 20, vituo vya afya vitano na kuhakikisha huduma za kibingwa zinapatikana katika hospitali ya wilaya. Pia aliahidi miradi ya maji kufikia asilimia 90 ya upatikanaji, pembejeo nafuu kwa wakulima na barabara za lami kilometa 120 ndani ya miaka mitano.

“Kwa mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi kusema CCM haijafanya lolote. Ukiona mtu anasema hivyo haraka sana muwahishe hospitali,” alisema kwa msisitizo.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Fantastic read! 👏 I really appreciate how clearly you explained the topic—your writing not only shows expertise but also makes the subject approachable for a wide audience. It’s rare to come across content that feels both insightful and practical at the same time. At explodingbrands.de we run a growing directory site in Germany that features businesses from many different categories. That’s why I truly value articles like yours, because they highlight how knowledge and visibility can create stronger connections between people, services, and opportunities.Keep up the great work—I’ll definitely be checking back for more of your insights! 🚀

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button