Dk Nchimbi kunguruma kampeni Tabora

TABORA; Mgombea mwenza wa urais kupitia CCM, Dk. Emmanuel Nchimbi, ameanza ziara yake mkoani Tabora leo Oktoba 4, 2025) akipokelewa kwa shamrashamra kubwa kutoka kwa maelfu ya wananchi.

Ziara hiyo ya siku tatu itamfikisha kwenye wilaya mbalimbali zikiwemo Sikonge, Kaliua na Igalula, ambako atakutana na wananchi, viongozi na kushiriki mikutano mikubwa ya kampeni.I



