Dk Nchimbi: Mchagueni Samia aendeleze maajabu

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakijawahi kupungukiwa viongozi wenye uwezo wa kutumikia Watanzania kwa ufanisi.
Mgombea mwenza wa urais kupitia CCM, Dk Emmanuel Nchimbi amesema hayo kwenye mkutano wa
kampeni mjini Handeni.
Dk Nchimbi amesema viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya rais hadi mwenyekiti wa kitongoji wanajua majukumu yao na wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wanapata huduma stahiki.
Amesema Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa kielelezo cha dhati cha dhamira hiyo kwa kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo katika kipindi cha miaka minne na nusu madarakani.
SOMA: CCM yaahidi stendi ya kisasa Mwanga
“Amefanya mambo makubwa katika sekta za afya, elimu, maji, barabara, kilimo na ufugaji. Ndiyo maana leo tunasema kwa kifua mbele, tumpe miaka mingine mitano ili azidi kutufanyia maajabu makubwa zaidi,” amesema Dk Nchimbi.
Ameongeza: “CCM ina viongozi wa kutosha wenye dhamira ya kweli ya kuwatumikia Watanzania. Kwa miaka mitano ijayo tuna uwezo, nia na dhamira ya kuyafanya makubwa zaidi”.
Dk Nchimbi amesema zaidi ya tani 1,175 za mbolea ya ruzuku zimetolewa kwa wakulima Handeni, huduma za ugani zimeimarishwa kupitia maofisa kilimo waliopatiwa zana za kisasa, na uzalishaji umeongezeka kutoka tani 59,320 hadi 72,326 katika kipindi cha miaka mitano.
Dk Nchimbi amesema serikali imeweka vifaa vya kupima udongo na kutoa usafiri kwa maofisa ugani ili kuongeza tija ya kilimo.
Katika sekta ya ufugaji alisema majosho mapya manne yamejengwa na kufanya Handeni kuwa na jumla ya majosho manane ya kisasa, huku mnada wa mifugo ukikarabatiwa ili kutoa huduma bora zaidi.
Kwa upande wa maji, miradi yenye thamani ya Sh bilioni 6.4 imekamilika na mipya ya zaidi ya Sh bilioni 14.3 inaendelea kutekelezwa.
Amesema barabara za lami Handeni zimeongezeka kutoka meta 400 hadi kilometa 4.7, barabara za changarawe kutoka kilometa 280 hadi kilometa 402, huku huduma za afya zikiboreshwa kupitia ujenzi wa zahanati mpya sita.
“Idadi ya watumishi wa afya Handeni imeongezeka kutoka 170 hadi 216, na shule mpya 10 za msingi, sekondari tano pamoja na madarasa zaidi ya 200 yamejengwa katika kipindi cha miaka mitano,” amesema.
Dk Nchimbi amesema katika miaka mitano ijayo serikali ya CCM itaboresha elimu Handeni kwa kuongeza idadi ya walimu na kujenga maabara za kisasa.
Alisema pia serikali itaimarisha barabara kwa kuongeza kilometa 400 za changarawe, kuweka taa za barabarani, kuanzisha miradi mipya ya maji katika vijiji 50 na kujenga vituo vitatu vya mabasi katika maeneo ya Mkata, Chogo na Chanika.
Kusemea Handeni mji bila kuonyesha mchango au hata picha ya mbunge wa jimbo hilo ni bayasi!
I am making a real GOOD MONEY ($100 to $120 / hr) online from my laptop. Last month I GOT cheek of nearly 19840$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. You become independent after joining this JOB. I really thanks to my FRIEND who refer me
This SITE….., http://Www.Cashprofit7.site
I have just received my 3rd payment order and $30,000 that I have built up on my laptop in a month through an online agent. This job is good and his regular salary is much better than my normal job.” Work now and start making money online yourself.
Go here…> t.ly/BmRZv