Dk Samia kuitikisa Pemba kampeni leo

PEMBA: MGOMBEA urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kutikisa kisiwa cha Pemba katika mwendelezo wa kampeni hii leo.
Tayari wananchi wanaendelea kumiminika katika viwanja vya Gombani ya Kale, Chake Chake, Pemba kusikiliza sera za CCM kupitia mgombea wake.
Mkutano wake wa kampeni visiwani Pemba unafuatiwa na mikutano miwili mikubwa iliyofanyika katika mikoa ya Kusini Unguja na Kaskazini Unguja, Visiwani Zanzibar ambako pamoja na mambo mengine alisisitiza amani na utulivu na kutoa ahadi za kwenda kufungua uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.



