Dk Tulia agusia sekta ya kilimo

MBEYA: KUIMARISHWA kwa usafiri wa reli na ujenzi wa uwanja wa kisasa wa maonyesho ya wakulima ya Nanenane jijini Mbeya kumetajwa kuwa kitakuwa kichocheo cha kukuza sekta ya kilimo na kuinua uchumi wa wakazi wa Jimbo la Uyole na maeneo jirani iwapo Chama Cha Mapinduzi(CCM) kitapewa ridhaa ya kuendelea kuwa madarakani.

Mgombea ubunge kupitia chama hicho katika Jimbo la Uyole, Dk Tulia Ackson ambaye pia ni Spika wa Bunge amebainisha hayo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Itezi uliopo Kata ya Nsalaga.

Dk Tulia amesema uzalishaji wa mazao ikiwemo mbogamboga na matunda unaofanyika katika jimbo la Uyole utaongezeka thamani iwapo serikali chini ya CCM itakamilisha uboreshaji wa miundombinu ya usafiri wa reli pamoja na Uwanja wa Nanenane.

Amesema Serikali imedhamiria kuimarisha miundombinu hiyo kwakuwa inatambua juhudi za uzalishaji mazao ya kilimo unaofanywa na wakazi wa Mkoa wa Mbeya wakiwemo wakazi wa Jimbo la Uyole.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button