DRC : Spika wa bunge ajiuzulu

DR CONGO : SPIKA wa Baraza la Chini la Bunge nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Vital Kamerhe, amejiuzulu kufuatia shinikizo kutoka kwa wabunge walioandaa hoja ya kumng’oa madarakani.

Kamerhe alichukua uamuzi huo kabla ya hoja hiyo kujadiliwa na kupigiwa kura bungeni. Wabunge pia walitaka viongozi wengine wanne wa ofisi ya bunge waondolewe kwa tuhuma za kushindwa kutekeleza majukumu. SOMA: DRC yazindua kampeni ya mauaji ya halaiki

Kujiuzulu kwake kunakuja wakati uhusiano kati ya Kamerhe na Rais Félix Tshisekedi ukiwa umedorora, tofauti na hapo awali walipokuwa wakishirikiana kisiasa.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button