DRC yazindua kampeni ya mauaji ya halaiki

GENEVA : SERIKALI ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imezindua kampeni katika Umoja wa Mataifa kutaka jumuiya ya kimataifa itambue kuwa mauaji yanayoendelea mashariki mwa nchi hiyo ni mauaji ya halaiki.
Waziri wa Haki za Binadamu wa DRC, Samuel Mbemba, alisema hayo jana katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Geneva, Uswisi, makao makuu ya Umoja wa Ulaya. SOMA: DRC, Rwanda zakubaliana kurejesha wakimbizi
Mbemba amesema hatua hiyo inalenga kuivunja dunia ukimya na kuhakikisha kuwa machafuko yanayoendelea mashariki mwa Congo yanatambuliwa rasmi kama mauaji ya halaiki. “Tumeanzia Geneva, na tutakwenda New York kuwatanabahisha viongozi watambue kwamba kinachotokea nchini mwetu ni mauaji ya halaiki,” alisema Mbemba.
Kampeni hiyo ya kidiplomasia inakuja wakati maelfu ya raia wa DRC wakiendelea kukimbia makazi yao kutokana na vita na mashambulizi yanayodaiwa kufanywa na makundi ya waasi, hali inayoongeza shinikizo kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua.
Google pays $300 on a regular basis. My latest salary check was $8600 for working 10 hours a week on the internet. My younger sibling has been averaging $19k for the last few months, and he constantly works approximately 24 hours. I’m not sure how simple it was once I checked it out.
This is my main concern……………………………. http://Www.Cash43.Com